14. Sehemu iliyoinuliwa katika Qur-aan

Allaah (Ta´ala) amesema:

وَجَعَلْنَا ابْنَ مَرْيَمَ وَأُمَّهُ آيَةً وَآوَيْنَاهُمَا إِلَىٰ رَبْوَةٍ ذَاتِ قَرَارٍ وَمَعِينٍ

“Tukamjaalia mwana wa Maryam na mama yake kuwa ni alama [kwa watu] na Tukawapa kimbilio katika sehemu iliyoinuka na penye utulivu na chemchemu za maji.”[1]

100- ´Ikrimah ameeleza kuwa Ibn ´Abbaas amesema kuhuiana na Aayah hii:

“Ni Dameski.”

Katika upokezi mwingine amesema:

“Ni mito ya Dameski.”

101- Mfano wa hayo yamepokelewa vilevile kutoka kwa Yahyaa al-Answaariy kutoka kwa Sa´iyd bin al-Musayyab kutoka kwake na Yahyaa kutoka kwa Sa´iyd kutoka kwa ´Abdullaah bin Salaam.

102- Sa´iyd amesema:

“Ni al-Ghuutwah Dameski.”

103- Katika upokezi mwingine amesema:

“Ni msikiti wa Dameski.”

104- Yaziyd bin Shajarah amesema:

“Dameski ndio sehemu iliyoinuka iliyobarikiwa.”

105- al-Hasan al-Baswriy amesema:

“Ndio ardhi ilio na miti na mito, yaani Dameski.”

Wengine waliosema kuwa ni Dameski ni Khaalid bin Ma´daan na Salaf wengine.

Kuna wengine waliosema kuwa ni Ramlah.

106- ´Abdur-Razzaaq amepokea kupitia kwa Bishr bin Raafiy´ ya kwamba Abu Hurayrah amesema kuhusiana na Aayah hiyo:

“Ni Ramlah Palestina.”

Hata hivyo Raafiy´ ni dhaifu katika Hadiyth.

Wanachuoni wengine wamesema sehemu iliyoinuka iliyotajwa katika Qur-aan ni Yerusalemu. Yamesemwa na Qataadah.

Kujengea maoni haya matatu sehemu iliyoinuka katika Qur-aan ni Shaam.

Baadhi wamesema kuwa iko Misri. Yamesemwa na Wahb bin Munabbih. Wengine wamesema kuwa iko Misri. Maoni hayo ni ya Zayd bin Aslam.

Baadhi ya wengine wamesema kuwa iko Kuufah. Haya ndio maoni dhaifu na mabaya kabisa. Maoni haya yamepokelewa na wanachuoni Kuufah kutoka kwa Shiy´ah kutoka kwa Ja´far as-Swaaqid na baba yake Abu Swaadiq.

[1] 23:50

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Baghdaadiy al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-ush-Shaam, uk. 117-121
  • Imechapishwa: 10/02/2017