14. Qadhwaa´ na Qadar ina daraja ngapi na ni zipi?


Swali 14: Imani ya kuamini Qadhwaa´ na Qadar ina daraja ngapi na ni zipi?

Jibu: Ni nne. Imani ya mtu haitimii mpaka aziamini zote:

1- Kuamini kuwa Allaah juu ya kila kitu ni mjuzi na ujuzi Wake umekizunguka kila kitu.

2- Kuamini kuwa ameyaandika yote hayo katika Ubao uliohifadhiwa.

3- Kuamini kuwa kila kinachopitika, basi kinapitika kwa matakwa na uwezo Wake. Anachotaka, huwa, na asichotaka, hakiwi.

4- Kuamini kuwa Allaah amewaacha waja watende kwa utashi wao. Wanatenda kwa khiyari yao wenyewe, kwa kutaka kwao na kwa nguvu zao. Allaah (Ta´ala) amesema:

أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ ۗ إِنَّ ذَٰلِكَ فِي كِتَابٍ ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرٌ

“Je, hujui kwamba Allaah Anajua yale yote yaliyomo katika mbingu na ardhi? Hakika hayo yameandikwa katika Kitabu. Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi.” (22:70)

لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَسْتَقِيمَ وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ

“Kwa yule atakaye miongoni mwenu anyooke. Na hamtotaka isipokuwa Atake Allaah, Mola wa walimwengu.” (81:28-29)