14. Njia ya saba: kuufanyisha ubongo mazoezi kuelewa na kuhifadhi

Miongoni mwa njia za kuitafuta elimu ni kufanyisha mazoezi ubongo kuelewa na kuhifadhi. Leo wanafunzi wamekosa jambo hili. Tunaona kuwa wanafunzi wengi hii leo wamezembea [kufanyisha mazoezi] ubongo wao na wamekuwa ni wenye kutegemea makaratasi. Wanahudhuria mizunguko ya elimu mingi, lakini wanafaidika kidogo. Kwa sababu utamkuta mmoja wao pindi anapohudhuria mzunguko wa kielimu anaishughulisha kalamu yake kuandika badala ya kushughulisha akili yake kwa yale anayoyasikia. Hatimae ikifika kesho ameyasahau. Isitoshe ni kwamba hafanyii marejeleo na kuhifadhi yaliyomo kwenye makaratasi haya. Hivyo anakuwa si mwenye kupata elimu. Matokeo yake anakuwa ameitoa elimu kutoka kwenye makaratasi kwenda kwenye makaratasi mengine kupitia njia ya mwalimu na wakati huo huo hakufaidika elimu yoyote. Ni jambo lisilokuwa na shaka kwamba kitendo hichi kinamfanya mwanafunzi kutopata elimu yoyote vovyote atakavyosoma, kuhudhuria [mizunguko ya elimu] na kusoma.

Mwanafunzi anatakiwa kuyafanya makaratasi kuwa ni njia ya kujithibitishia elimu kwenye nafsi yake na aufanyishe mazoezi ubongo wa kuyaelewa na kuyahifadhi yaliyosemwa.

 

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Ilm wa Wasaaailuh wa Thimaaruh
  • Imechapishwa: 22/10/2016