Yakishabainika haya ni lazima kutambua ni kina nani wanachuoni wa kweli – amnao ni wale walezi ambao huwalea watu juu ya Shari´ah ya Mola wao – ili waweze kubainika kutokamana na wale wanaojifananisha nao ilihali si katika wao. Wanajifanananisha nao katika muonekano, matendo na maneno. Lakini hata hivyo si miongoni mwao juu ya kuwatakia watu kheri na kuitaka haki. Kubwa walonalo ni kuivisha haki batili na kuirembaremba kwa maneno ya kupambapamba ambapo yule mwenye kiu hufikiri kuwa ni maji lakini anapofika hapati kitu. Bali si vyenginevyo isipokuwa ni uzushi na upotofu ambayo baadhi ya watu hufikiria kuwa ndio elimu na Fiqh na kwamba hakuna anayesema mengine isipokuwa zandiki au mwendawazimu. Haya ndio maana ya maneno ya mwanachuoni (Rahimahu Allaah). Ni kama kwamba anawaashiria viongozi wa wazushi wenye kupotosha ambao huwatuhumu maimamu wa Ahl-us-Sunnah kwa mambo ambayo wako mbali nayo. Lengo lao watu wakimbie mbali kuchukua elimu kwao. Huu ni urithi waliorithi kutoka kwa wale waliochupa mpaka kabla yao na wakawakadhibisha Mitume. Allaah (Ta´ala) amesema:

كَذَٰلِكَ مَا أَتَى الَّذِينَ مِن قَبْلِهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا قَالُوا سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ أَتَوَاصَوْا بِهِ ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ طَاغُونَ

“Ndio kama hivyo, hawakuwafikia wale wa kabla yao Mtume yoyote isipokuwa walisema “Mchawi au mwendawazimu”. Je, wameusiana kwa hayo? Bali wao ni watu wenye kuvuka mpaka.”[1]

[1] 51:53

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sittah, uk. 24-25
  • Imechapishwa: 22/06/2021