14. Mwenye janaba kufanya Tayammum badala ya wudhuu´


12- Mwenye janaba kufanya Tayammum badala ya wudhuu´

Inafaa kwao wakati mwingine kufanya Tayammum badala ya wudhuu´ kutokana na Hadiyth ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye amesimulia:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa anapata janaba na akataka kulala basi anatawadha au anafanya Tayammum.”[1]

[1] Ameipokea al-Bayhaqiy (01/200) kupitia njia ya ´Uthmaan bin ´Aliy ambaye kapokea kutoka kwa Hishaam  ambaye na yeye kapokea kutoka kwa baba yake. al-Haafidhw amesema:

“Mlolongo wa wapokezi wake ni mzuri.” (al-Fath (01/313)).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 117-118
  • Imechapishwa: 10/03/2018