Miongoni mwa misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni uharamu wa kuwafanyia uasi watawala wa waislamu wanapofanya makosa yaliyo chini ya kufuru kutokana na amri yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kuwatii katika mema muda wa kuwa hawajafanya kufuru ya wazi. Hilo ni tofauti na wanavyofanya Mu´tazilah ambao wanaonelea kuwa ni wajibu kufanya uasi dhidi ya viongozi pindi wanapofanya dhambi kubwa hata kama itakuwa sio kufuru. Wanaonelea kuwa kufanya hivo ni katika kuamrisha mema na kukataza maovu. Uhakika wa mambo ni kuwa kitendo hichi cha Mu´tazilah ndio uovu mkubwa. Kwa sababu kinapelekea katika khatari kubwa ya vurugu, mambo kuharibika, umoja kuharibika na maadui kupata fursa ya kuvamia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Usuwl ´Aqiydah Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 31
  • Imechapishwa: 12/05/2022