Tawhiyd ina fadhilah nyingi, jambo ambalo linatambulika kwa wanafunzi na mlinganizi. Miongoni mwa fadhilah zake ni pamoja na:

1- Inamfanya mtu kutodumishwa Motoni milele muda wa kuwa moyoni mwake kuna chembe kidogo ya mbegu ya hardali.

2- Ikikamilika ndani ya moyo basi inamzuia mtu kuingia Motoni kabisa.

3- Mtu akiihakikisha basi anapata uongofu na amani kamilifu duniani na Aakhirah[1].

4- Ambaye ana furaha zaidi ya uombezi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni yule mwenye kusema:

“Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah” hali ya kuwa ni msafi kutoka moyoni mwake[2].

5- Matendo na maneno yenye kuonekana na yaliyojificha inapokuja katika kukubaliwa kwake, ukamilifu wake na kulipwa kwa wingi kunategemea na Tawhiyd ya mtu. Kila ambavo inakuwa ni yenye nguvu zaidi basi yanakamilika mambo haya.

6- Kunamfanya mtu kuwa huru kutoka katika utumwa wa viumbe, kuwategemea, kuwaogopa, kuwa na matarajio kwao na kufanya matendo kwa sababu yao. Huu ndio utukufu wa kikweli…

Zipo faida nyenginezo nyingi ambazo ameziashiria Shaykh Ibn-us-Sa´diy katika maelezo yake ya chini ya “Kitaab-ut-Tawhiyd”[3].

[1] Amesema (Ta´ala):

الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ أُولَـٰئِكَ لَهُمُ الْأَمْنُ وَهُم مُّهْتَدُونَ

“Wale walioamini na hawakuchanganya imani zao na dhuluma, hao ndio watakaopata amani nao ndio walioongoka.” (06:82)

[2] al-Bukhaariy (99).

[3] ”al-Qawl-us-Sadiyd fiy Maqaaswid-it-Tawhiyd”, uk. 23-24.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Usuwl-ud-Da´wah as-Salafiyyah, uk. 43-44
  • Imechapishwa: 06/08/2020