14. Mfano wa tisa kuonyesha jinsi Raafidhwah wanavodai kuwa Maswahabah wamepotosha Qur-aan

Msiba wa msiba ni yale yaliyokuja kwa al-Kulayniy pale aliposema katika “al-Kaafiy”[1]:

“´Aliy bin al-Hakam amepokea kutoka kwa Hishaam bin Saalim, kutoka kwa Abu ´Abdillaah ambaye amesema:

“Qur-aan ambayo Jibriyl (´alayhis-Salaam) alikuja nayo kwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ina Aayah 17.000.”

Malengo ya mapokezi haya ni kwamba Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wameondosha Aayah 10.334 kwenye Qur-aan. Ni jambo lenye kujulikana ya kwamba Qur-aan ina Aayah 6666. Hii ina maana ya kwamba waliondosha sehemu kubwa ya Qur-aan. Kwa nini walifanya hivo? Ni kwa sababu wanawachukia watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Raafidhwah Baatwiniyyah wanasema uongo! Ni wingi ulioje wanavomsemea uongo Allaah, Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] 02/634

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 42
  • Imechapishwa: 19/03/2017