14. Matakwa ya mwanadamu hayatoki nje ya matakwa ya Allaah

Haya hayazuii mja kuwa na matakwa na utashi, akawa ni mwenye khiyari ima ya kufanya au kuacha jambo, uwezo wa kufanya au kuliacha jambo. Kwa msaada wa hayo ana uwezo wa kuchagua kati ya mambo yenye kudhuru na yenye kunufaisha.

Mja anafanya mema, mazuri na utiifu kwa utashi wake kama ambavyo kwa utashi wake vilevile anaacha utiifu na mambo ya wajibu. Kwa utashi wake ndio anafanya maasi na madhambi. Atafanyiwa hesabu kwa mujibu wa matakwa na matendo yake. Pamoja na haya yote matakwa na utashi wake havitoki nje ya matakwa ya Allaah. Amesema (Ta´ala):

وَمَا تَشَاؤُونَ إِلَّا أَن يَشَاء اللَّهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ

“Wala nyinyi hamtataka isipokuwa atake Allaah, Mola wa walimwengu wote.”[1]

Amemthibitishia mja kuwa na matakwa. Lakini hata hivyo ameyaambatanisha na matakwa na utashi Wake (Subhaanahu wa Ta´ala). Kwa ajili hii pindi mtu alipomwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kama alivyotaka Allaah na wewe” akamwambia: “Je, umenifanya kuwa ni mwenza wa Allaah?” Sema: “Kama alivyotaka Allaah kisha ukataka wewe” au alisema: “Kama alivyotaka Allaah peke yake.”[2]

[1] 81:29

[2] Ibn Maajah (2117) na Ahmad (01/214).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mujmal ´Aqiydat-is-Salaf as-Swaalih, uk. 14
  • Imechapishwa: 24/05/2022