2- Daku imependekezwa. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ

“Kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu uzi mweupe wa alfajiri kutokana na uzi mweusi.”[1]

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia kwa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa na waadhini wawili; Bilaal na Ibn Umm Maktuum ambaye alikuwa kipofu ambapo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Bilaal anaadhini usiku. Hivyo kuleni na kunyweni mpaka aadhini Ibn Umm Maktuum.”

Qaasim bin Muhammad – ambaye ni mmoja wa wapokezi wa Hadiyth hiyo – amesema:

“Hakukuwa na kitambo kirefu baina ya muadhini wa kwanza na wa pili.”[2]

Miongoni mwa dalili za kwamba daku imependekezwa ni yale yaliyothibiti kwa al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa Anas (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kuleni daku. Kwani katika daku kuna baraka.”[3]

3- Imependekezwa kuichelewesha daku. Hayo ni kutokana na yale yaliyopokelewa katika “as-Swahiyh” ya Muslim kupitia kwa ´Amr bin al-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kipambanuzi kati ya swawm yetu na swawm ya Ahl-ul-Kitaab ni kula daku.”[4]

[1] 02:187

[2] al-Bukhaariy (617) na Muslim (1092).

[3] al-Bukhaariy (1923) na Muslim (1095).

[4] Muslim (1096).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtaswaru fiy Ahkaam-is-Swiyaam, uk. 19-21
  • Imechapishwa: 23/05/2019