14- Madhambi yanamfanya Allaah kumdharau mja Wake


Madhambi yanamfanya yule mtenda dhambi kumchukua wepesi Allaah na Allaah anamuona mja wake huyo mbele ya macho Yake si lolote si chochote. al-Hasan al-Baswriy amesema:

“Aliwaona si lolote si chochote ndipo wakamuasi. Lau angeliwatukuza basi Angeliwakinga.”

Allaah akimtweza mtu basi hakuna yeyote awezaye kumtukuza. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَن يُهِنِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِن مُّكْرِمٍ

“Ambaye Allaah amemtweza, basi hatopata yeyote wa kumtukuza.”[1]

Hata kama kwa uinje watu watawatukuza kwa sababu ni wenye kuwahitajia au kwa sababu ya kuchelea shari zao, basi ndani ya nyoyo zao wao ndio wenye kutwezwa na wenye kudharauliwa zaidi.

[1] 22:18

  • Mhusika: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Daa’ wad-Dawaa’, uk. 70
  • Imechapishwa: 07/01/2018