Imaam al-Barbahaariy (Rahimahu Allaah) amesema:

Mwenye kwenda kinyume na Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika jambo la dini, amekufuru.

MAELEZO

Kukufuru hapa inawezekana ikawa ni kufuru kubwa au ndogo. Itategemea na kwenda kinyume kwenyewe. Amekufuru haina maana kwamba amekufuru kufuru yenye kumtoa katika Uislamu pasi na kufungamanisha. Kuna uwezekano ikawa ni hivi au kufuru ndogo. Muhimu ni kuwa kwenda kinyume na Salaf ni kufuru. Kuna uwezekano ikawa ni kubwa au ndogo kutegemea na  kwenda kinyume kwenyewe.

Makusudio vilevile inaweza kuwa atapoenda kinyume nao katika jambo dogo la dini basi hatua kwa hatua ataenda anafanya hivo mpaka ajikute ametoka katika dini kabisa. Hatimaye jambo lake limpelekee katika kufuru. Akiendelea kwenda kinyume hatimaye jambo lake litampelekea katika kufuru kubwa. Hatimaye atoke katika dini kabisa. Shaytwaan, matamanio na nafsi itaenda naye hatua kwa hatua mpaka mwishoni atoke katika dini moja kwa moja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Sharh-is-Sunnah, uk. 33-34
  • Imechapishwa: 23/10/2017