14. Khawaarij na Murji-ah wamepotea kwa sababu hii

Kuvijua vitenguzi hivi kuna umuhimu mkubwa ili mtu awe juu ya utambuzi na asije kuwa pamoja na Khawaarij wala asiwe pamoja na Murji-ah. Bali anatakiwa awe pamoja na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ambao wameoanisha kati ya maandiko kwa kuyatendea kazi maneno Yake (Ta´ala):

هُوَ الَّذِي أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ ۖ فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ

”Yeye ndiye ambaye kakuteremshia Kitabu humo mna Aaya zilizo wazi – hizo ndio msingi wa Kitabu – na nyinginezo ni [Aayah] zisizokuwa wazi. Ama wale ambao nyoyoni mwao mna upotevu hutafuta zile zisizokuwa wazi kwa lengo la kutaka fitina na kutaka kuzipotosha.” (Aal ´Imraan 03:07)

Wale ambao ndani ya nyoyo zao mna upotofu ndio Khawaarij na Murji-ah. Khawaarij wamechukua zile Aayah zisizokuwa wazi. Murji-ah pia wamechukua zile Aayah zisizokuwa wazi. Wote wawili hawakurudisha Aayah zisizokuwa wazi katika zile Aayah zisizokuwa wazi. Kwa sababu Qur-aan inajifasiri na kujibainisha yenyewe. Ama Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na wale waliobobea katika elimu wamechukua yote mawili ambapo wamerudisha Aayah zisizokuwa wazi kwenda zile zilizo wazi na wakafasiri Aayah zisizokuwa wazi kwa zile zilizo wazi na mwishowe wakaongoka katika haki:

وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا

“Wale waliobobea katika elimu husema: “Tumeziamini – zote ni kutoka kwa Mola wetu.”[1]

bi maana zote zisizokuwa wazi na zilizo wazi.

Maneno ya Allaah hayagongani. Kadhalika maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hayagongani. Wamekusanya kati ya hayo mawili, wakafasiri hiki kwa kile na wakakitilia kanuni hiki kwa kile. Huu ndio mfumo wa wale waliobobea katika elimu.

Ama wapotevu wao wamechukua upande mmoja ambao ni zile Aayah zisizokuwa wazi.

Aayah zisizokuwa wazi katika zile za ahadi zimechukuliwa na Murji-ah. Aayah zisizokuwa wazi katika zile za matishio zimechukuliwa na na Khawaarij. Hatimaye wakawa wamepokea kutoka katika njia iliyonyooka.

[1] 03:07

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 27-28f
  • Imechapishwa: 08/05/2018