3- Kujitapisha. Ni kule kutoa kilichomo tumboni katika chakula au kinywa kwa kukusudia kupitia njia ya mdomo. Lakini mtu yakimshinda matapishi na yakamtoka bila yeye kutaka, jambo hilo haliathiri swawm yake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ambaye yatamshinda matapishi hakuna juu yake kulipa na ambaye atajitapisha basi alipe.”[1]

[1] Abu Daawuud (2380), at-Tirmidhiy (720) na Ibn Maajah (1676). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Ibn MAajah” (1368).

  • Mhusika: Nukhbatin minal-´Ulamaa´
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fiqh-ul-Muyassar, uk. 158
  • Imechapishwa: 25/04/2020