Sitaki kuwarefushia. Hizi ni baadhi ya sababu zinazofanya familia kupata furaha. Nimezitoa katika Kitabu cha Mola Wetu na katika Sunnah za Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kutarajia tutazitendea kazi, kuzifunza na kuzieneza ili familia ziweze kupata utulivu na furaha na kuwaondoa mashaytwaan kutoka katika majumba yetu.’

Napenda kukhitimisha kwa wasia: tuviweke mbali vile vinavyomghadhibisha Allaah kutoka majumbani mwetu. Ninaapa kwa Allaah miongoni mwa sababu kubwa za kukosa furaha ni kuweka majumbani mwetu vitu vinavyomkasirisha Allaah. Haijalishi kitu hata kama watu watafikiri kuwa ni katika sababu za kupata furaha.

Ndugu wapendwa! Ni lazima kwetu kuyatazama manyumba yetu. Tukipata ndani yake kuwa kuna mambo yanayomkasirisha Allaah basi tuyaondoe kutoka nyumbani. Hayo yatatufanya kuihakikisha furaha. Ndugu wapendwa! Ala ala zingatieni jambo hili kubwa.

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Asbaab sa´aadat-il-Usrah, uk. 44-45
  • Imechapishwa: 15/10/2016