Swali 14: Kupata hedhi mchana wa Ramadhaan ni jambo linaiathiri funga ya mwanamke?

Jibu: Damu ya hedhi ikimtoka mwanamke basi swamw yake inaharibika. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Je, mwanamke anapopata hedhi si haswali wala hafungi?”

Kwa hivyo tunazingatia jambo hilo ni katika vifunguzi. Hukumu hiyohiyo inazingatiwa juu ya damu ya uzazi.

Kutokwa na damu ya hedhi na damu ya uzazi kunaiharibu swawm. Mjamzito kutokwa na damu mchana wa Ramadhaan, ikiwa ni hedhi basi inazingatiwa hukumu moja kama hedhi, licha ya kwamba mjamzito hapati hedhi. Bi maana tunakusudia kwamba damu hiyo inaathiri funga yake. Ikiwa sio hedhi basi haiathiri. Hedhi anayoweza kupata mjamzito ni ile ambayo damu ambayo haikuzuka katikati na haikukatika tangu aliposhika mimba. Bali damu hiyo ilikuwa inamjia katika zile nyakati zake zilizozoeleka. Hii itakuwa ni hedhi kwa mujibu wa maoni yaliyo na nguvu. Damu hiyo itakuwa na hukumu moja kama ya hedhi. Lakini ikiwa damu imemkatika kisha baadaye akawa anaona damu ambayo si yenye kuzoeleka. Basi damu hii haiathiri funga yake kwa sababu haihesabiki kuwa ni hedhi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 15-16
  • Imechapishwa: 23/06/2021