Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

9- Mawazo hayawezi kumfikia, fahamu haziwezi kumzunguka Yeye.

MAELEZO

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) hawezi kuzungukwa. Yeye ni mkubwa kabisa kuliko kila kitu:

يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يُحِيطُونَ بِهِ عِلْمًا

“Anajua yale yaliyoko mbele yao na yale yaliyoko nyuma yao na wala hawawezi kumzunguka Yeye wote kiujuzi.”[1]

Upande mmoja kuna elimu kumuhusu Allaah. Upande mwingine hawezi kuzungukwa. Yeye ni mkubwa kuliko kila kitu. Mawazo hayawezi kumfikiria. Wala haijuzu kusema kitu kumuhusu isipokuwa yale yaliyosemwa na Allaah (Subhaanah) au yakasemwa na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] 20:110

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 37
  • Imechapishwa: 11/09/2019