189 – Abu Maalik al-Ash´ariy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Twahara ni nusu ya imani. Kusema “Himdi zote njema anastahiki Allaah (الحمد لله) kunajaza mizani, na kusema “Allaah ametakasika na mapungufu, na himdi zote njema anastahiki Allaah (سبحان الله والحمد لله) kunajaza yaliyomo kati ya mbingu na ardhi. Swalah ni nuru, swadaqah ni hoja, subira ni mwanga na Qur-aan ni ima hoja yako au dhidi yako. Kila mmoja ni mwenye kujipinda na kuiuza nafsi yake; ima akaiacha huru au akaiangamiza.”

Ameipokea Muslim, at-Tirmidhiy na Ibn Maajah ambaye yeye amesema:

“Kueneza vizuri wudhuu´ ni nusu ya imani.”

Ameipokea pia an-Nasaa´iy pasi na “Kila mmoja ni mwenye kujipinda… “

Haafidhw ´Abdul-´Adhwiym amesema:

Nimeandika kitabu cha kujitegemea juu ya cheni za wapokezi za Hadiyth hii, hekima na faida zake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/194)
  • Imechapishwa: 14/04/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy