14. Hadiyth “Atakayefunga siku moja katika njia ya Allaah, basi Allaah ataweka kati yake yeye na Moto… “


991- Abu Umaamah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayefunga siku moja katika njia ya Allaah, basi Allaah ataweka kati yake yeye na Moto kama mfano wa masafa kati ya mbingu na ardhi.”[1]

Ameipokea at-Tirmidhiy kupitia kwa al-Waliyd bin Jamiyl, kutoka kwa Qaasim bin ´Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Abu Umaamah. at-Tirmidhiy amesema:

“Hadiyth geni.”

Wanachuoni wengi wanaonelea kuwa Hadiyth hizi zinahusiana na fadhilah za kufunga katika Jihaad, jambo ambalo at-Tirmidhiy na wengineo wameliwekea mlango. Wanachuoni wengine wameonelea kuwa kila swawm inayofungwa kwa ajili ya Allaah ni katika njia ya Allaah.

[1] Nzuri kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (01/581)
  • Imechapishwa: 06/06/2018
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy