as-Sufrah ni kitu kama usaha ambacho juu yake kunakuwa rangi ya manjano.

al-Kudrah ni kitu kama rangi ya maji machafumachafu yenye rangi ya kijivu.

Mwanamke akitokwa na rangi ya manjano au machafumachafu yenye rangi ya kijivu katika wakati wa ada yake, basi ataizingatia kuwa ni hedhi ambayo itachukua hukumu zake zilizotangulia. Rangi hii ikimtoka mwanamke mbali na ule wakati wa ada yake, basi haitozingatia chochote na atajizingatia kuwa ni msafi. Umm ´Atwiyyah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Tulikuwa hatuzingatii umanjano na uchafuchafu wa kijivu baada ya kutwaharika kuwa ni kitu.”

Maneno haya hukumu yake ni yenye kurufaishwa kwa mujibu wa wanazuoni wa Hadiyth. Kwa sababu yanazingatiwa ni uthibitisho kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kinachopata kufahamika ni kwamba ile rangi ya kijivu na umanjano kabla ya twahara ni hedhi na inachukua hukumu yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 30
  • Imechapishwa: 28/10/2019