Swali 14: Ni jambo linalojulikana ya kwamba kulingania kwa Allaah ni kitu kinachohitajia elimu ya Kishari´ah. Je, kinachozingatiwa ni kuhifadhi Qur-aan na Sunnah? Je, inatosha ile elimu ambayo mtu anasoma katika mashule na katika vyuo vikuu?

Jibu: Elimu inahusiana na mtu kuhifadhi maandiko na kuelewa maana yake. Haitoshelezi kuhifadhi maandiko peke yake. Haitoshi kwa mtu akahifadhi maandiko ya Qur-aan na Sunnah. Ni lazima kwa mtu kufahamu maana yake sahihi. Kuhifadhi peke yake pasi na kuelewa maana yake haimstahikii yeyote kulingania kwa Allaah (´Azza wa Jall).

Ama yale yanayosomwa katika mashule, ni yenye kutosha ikiwa yanahusiana na kuhifadhi maandiko na kufahamu maana yake. Lakini ikiwa inahusiana na kuhifadhi maandiko peke yake pasi na kuelewa maana yake, hili halistahikii kulingania. Hata hivyo inawezekana kuwahifadhisha wanafunzi maandiko pasi na kuwafafanulia maana yake au kuwasomea na kuwasikilizisha nayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 39-40
  • Imechapishwa: 31/05/2023
  • mkusanyaji: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy