Tunamshukuru Allaah ipo Aayah tunayoisoma kwenye Qur-aan. Amesema (Ta´ala):

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا

 “Leo wamekata tamaa wale waliokufuru juu ya dini yenu, hivyo basi msiwaogope na niogopeni Mimi. Leo nimekukamilishieni dini yenu na nimekutimizieni neema Yangu na nimekuridhieni Uislamu uwe dini yenu.”[1]

Lau katika mambo yanayozuliwa yangelikuwepo ambayo yanaifanya dini kukamilika basi yangeliwekwa katika Shari´ah, yakafikishwa na kuhifadhiwa. Lakini ndani yake hakuna kitu kinachofanya dini kukamilika. Bali ni kufanya upungufu katika dini ya Allaah.

Huenda mtu akasema kwamba katika hayo mambo yaliyozuliwa tunapata hisia za kidini, mioyo kutikisika [kwa kumcha Allaah] na tunakuwa na umoja. Tunawajibu kwa kusema kwamba Allaah ameeleza kuwa shaytwaan amesema:

ثُمَّ لَآتِيَنَّهُم مِّن بَيْنِ أَيْدِيهِمْ وَمِنْ خَلْفِهِمْ وَعَنْ أَيْمَانِهِمْ وَعَن شَمَائِلِهِمْ

“Kisha nitawaendea mbele yao na nyuma na kuliani kwao na kushotoni kwao.”[2]

Shaytwaan ndiye mwenye kuyapamba kwenye moyo wa mtu kwa lengo la kumzuia na ´ibaadah ya Allaah alizomuwekea. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameeleza ya kwamba:

“Shaytwaan hutembea ndani ya mwanadamu kama damu inavyotembea.”[3]

[1] 05:03

[2] 07:17

[3] al-Bukhaariy (2035) na Muslim (2175).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy-´Aqiydah wal-´Amal, uk. 24-25
  • Imechapishwa: 25/07/2019