14. Daraja ya nne ya makadirio: Kuumba

Daraja ya nne: Kuumba. Tunaamini kuwa Allaah (Ta´ala) ndiye muumba wa kila kitu. Hakuna kilichopo mbinguni wala ardhini isipokuwa Allaah amekiumba. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) ameyaumba mpaka mauti hata kama mauti yenyewe hayana uhai. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

الَّذِي خَلَقَ الْمَوْتَ وَالْحَيَاةَ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا

“Ambaye ameumba mauti na uhai ili akujaribuni ni nani kati yenu aliye na matendo mema zaidi.” [1]

Kila kilichopo mbinguni na ardhini basi Allaah (Ta´ala) ndiye amekiumba. Hakuna muumba mwingine isipokuwa Allaah (Tabaarak wa Ta´ala). Tunajua kuwa kila kile (Subhaanah) anachofanya ni kiumbe Chake. Milima, ardhi, mito, jua, mwezi, nyota, upepo, mwanaadamu na wanyama vyote vimeumbwa na Allaah. Sifa za viumbe hivi na kubadilika kwa hali zavyo pia vimeumbwa na Allaah.

[1] 67:02

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Qadhwaa’ wal-Qadar, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (5/225)
  • Imechapishwa: 25/10/2016