13. Dalili ya mipango na makadirio kutoka katika Qur-aan na Sunnah

Mipango na makadirio ni kitu kimethibiti katika Qur-aan na Sunnah. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ فَقَدَّرَهُ تَقْدِيرًا

“Ameumba kila kitu akakikadiria kiwango cha sawasawa.”[1]

إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ

”Hakika sisi Tumekiumba kila kitu kwa Qadar.”[2]

وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ

”Hamtotaka isipokuwa atake Allaah, Mola wa walimwengu.”[3]

Katika Sunnah ni Hadiyth ya Jibriyl pindi alipomwambia Mtume (Swall Allaahu ´alayhi wa sallam): “Nieleze kuhusu imani?” Akasema:

“Imani ni kumwamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Yake, siku ya Mwisho na kuamini Qadar kheri na shari yake.”

[1] 25:02

[2] 54:49

[3] 81:29

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 32
  • Imechapishwa: 04/03/2021