14. Dalili ya kuwa mwenye kumuasi Mtume (صلى الله عليه وسلم) ataingia Motoni

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

… na yule mwenye kumuasi, ataingia Motoni. Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّا أَرْسَلْنَا إِلَيْكُمْ رَسُولًا شَاهِدًا عَلَيْكُمْ كَمَا أَرْسَلْنَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ رَسُولًا فَعَصَىٰ فِرْعَوْنُ الرَّسُولَ فَأَخَذْنَاهُ أَخْذًا وَبِيلًا

“Hakika Sisi tumekutumieni Mtume awe shahidi juu yenu, kama tulivyotuma kwa Fir’awn Mtume. Lakini Fir’awn alimuasi huyo Mtume tukamchukuwa mchukuo wa kuangamiza.” (al-Muzzammil 73 : 15-16)

MAELEZO

Hili pia ni haki na yamechukuliwa kutoka katika maneno Yake (Ta´ala):

وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَيَتَعَدَّ حُدُودَهُ يُدْخِلْهُ نَارًا خَالِدًا فِيهَا وَلَهُ عَذَابٌ مُّهِينٌ

“Na yeyote atakayemuasi Allaah na Mtume Wake na akapindukia mipaka Yake atamwingiza Motoni, ni mwenye kudumu humo na atapata adhabu inayodhalilisha.” (an-Nisaa´ 04 : 14)

وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا

“Na anayemuasi Allaah na Mtume Wake, basi kwa hakika amepotea upotofu wa wazi.” (al-Ahzaab 33 : 36)

وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَإِنَّ لَهُ نَارَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا

“Na yeyote yule atakayemwasi Allaah na Mtume Wake, basi hakika atapata Moto wa Jahannam, ni wenye kudumu humo milele.” (al-Jinn 72 : 23)

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth iliyotangulia:

“… na yule atayeniasi ataingia Motoni.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 33
  • Imechapishwa: 18/05/2020