14. Dalili ya kumi na mbili kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe

12- Abu Sa´iyd al-Khaliyl bin Abiyr-Rajaa’ ar-Raaraaniy ametuhadithia: Abu ´Aliy al-Haddaad ametuhadithia: Abu Nu´aym ametuhadithia: Abu Bakr bin Abiy Khallaad ametuhadithia: al-Haarith bin Muhammad bin Abiy Usaamah ametuhadithia: Ahmad bin Yuunus ametuhadithia: Abul-Haarith al-Warraaq ametuhadithia, kutoka kwa Bakr bin Khunays, kutoka kwa Muhammad bin Sa´iyd, kutoka kwa ´Ubaadah bin Nusayy, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Ghunm, kutoka kwa Mu´aadh bin Jabal ambaye ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika Allaah anachukia mbinguni Abu Bakr kuchukiwa ardhini.”[1]

[1] Ibn-ul-Jawziy amesema:

“Hadiyth hizi amezuliwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakuna anayepokea kutoka kwa Bakr bin Khunays isipokuwa ni Abul-Haarith ambaye anaitwa Naswr bin Hammaad. Yahyaa amesema: “Ni mwongo.” Muslim al-Hajjaaj amesema: “Hadiyth zake si lolote si chochote.” an-Nasaa´iy amesema: “Sio mwaminifu.”” (al-Mawdhuu´aat (1/319))

adh-Dhahabiy amesema:

“Abul-Haarith hajulikani. Bakr ni dhaifu. Mwalimu mwenye kusulubiwa ameharibika. Khabari si sahihi. Allaah amlaani yule mwenye kumchukia Abu Bakr!” (al-´Uluww, uk. 55)

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 84-85
  • Imechapishwa: 02/06/2018