Swali 14: Mara nyingi napitwa na swalah na naikusanya na ile ya baada yake. Hayo yanakuwa kwa sababu ya kazi nyingi katika uuguzi au kuwafanyia uchunguzi wagonjwa. Kadhalika napitwa na swalah ya ijumaa kwa ajili ya kuwahudumikia wagonjwa. Je, kitendo hichi kinafaa?

Jibu: Lililo la wajibu ni kuswali swalah kwa wakati wake. Haifai kuchelewesha kutoka wakati wake. Kuhusu swalah ya ijumaa ukiwa ni mlinzi au mfano wake miongoni mwa wale ambao hawawezi kuswali ijumaa pamoja na wengine basi inadondoka kwako na uswali Dhuhr kama mgonjwa na mfano wake. Ama swalah zengine ni lazima kwako kuziswali ndani ya wakati wake. Haifai kujumuisha baina ya swalah mbili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Mariydhw, uk. 35-36
  • Imechapishwa: 10/07/2019