14- Wanafanya utatizi na kujadili sana pindi mtu anapowaambia kuachana na makosa ya wazi yaliyoko katika mfumo wa al-Ikhwaan al-Muslimuun ambayo kwa mujibu wao hayana makosa. Jibu lao ni kuwa wanaapa kwa Allaah kwa kukariri ili kuitakasa njia yao, kupinga kila kibaya kilichofungamana na mfumo na kuuthibitishia kila zuri. Hapo ndipo mlinganiaji na mwenye kuwatamania watu kheri humwacha Allaah asimamie jambo lao.

Kuhusiana na wale ambao hawana ujuzi juu ya mfumo huu, sheria zake, viongozi wake na nadharia yake, wanatumbukia kwenye shimo lake kama jinsi kipepeo kinavyohadaika na mwanga wa moto hatimae kinatumbukia moja kwa moja ndani ya moto. Kwa sababu udhahiri wao ni kuwa wako na ghera juu ya Shari´ah ya Kiislamu, wakati undani wao wana hila, njama na kutamani kumpoteza kila ambaye anasapoti mfumo wa Salaf au kuwapenda kwa sababu ameshikamana na Kitabu cha Mola Wao (´Azza wa Jall), Sunnah Swahiyh za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa mujibu wa uelewa wa Salaf.[1]

[1] Imaam Swaalih al-Fawzaan amesema:

“Kijitabu hichi kilichoko mbele yetu kimeandikwa na ndugu yetu Shaykh Zayd bin Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy. Kinatahadharisha mifumo hii, kinabainisha athari zake mbaya na kinahimiza kushikamana barabara na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Allaah amjaze kheri na anufaishe kwa nasaha na maelekezo yake.” (Asbaab Istiqaamat-ish-Shabaab wa Bawaa´ith Inhiraafihim, uk. 7)

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Asbaab Istiqaamat-ish-Shabaab wa Bawaa´ith Inhiraafihim, uk. 21
  • Imechapishwa: 25/03/2017