63. Uthibitisho ya kwamba shirki ya watu wa kale ni khafifu kuliko shirki ya watu wa zama zetu III

Jambo la pili: Watu wa mwanzo walikuwa wakiomba pamoja na Allaah watu waliokuwa karibu na Allaah. Ima Mitume, mawalii au Malaika. Na wanaomba pia miti au mawe vinavyomtii Allaah na havimuasi. Lakini watu wa zama zetu wanaomba pamoja na Allaah katika mafusaki ya watu. Na wale wanaowaomba ndio wanaowahalalishia maovu kama vile zinaa, kuiba, kuacha swalah na mengineyo.

MAELEZO

Jambo la pili: Tofauti ya pili ni kwamba washirikina wa mwanzo walikuwa wakiwaomba watu waliokuwa na kitu katika wema na kujikurubisha kwa Allaah katika Malaika, Mitume na waja wema au wanaomba miti au mawe vitu ambavyo havimuasi Allaah.

Kuhusu washirikina waliokuja nyuma wanawaomba viumbe waovu kabisa na walio na kufuru na dhambi zaidi na wale wanaodai ya kwamba wana karama na kwamba ´ibaadah sio yenye kuwawajibikia miongoni mwa wakanamungu katika Suufiyyah ambao wanawahalalishia mambo ya haramu na wanaacha mambo ya wajibu. Miongoni mwa hao ni kama al-Badawiy, al-Hallaaj, Ibn ´Arabiy na viongozi wengine wa ukafiri. Wanawaomba ilihali wanashuhudia kuwa wanafanya machafu na wanaacha mambo ya faradhi na wanadai kuwa wayafanyayo ni karama na fadhila zao kwa kuwa ´ibaadah sio yenye kuwawawajibikia tena.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 94
  • Imechapishwa: 30/01/2017