138. Kwa nini Khidhr hakumfuata Muusa (´alayhis-Salaam)?

Kwa nini Khidhr hakumfuata Muusa (´alayhis-Salaam)?

Jawabu ni kwamba Muusa (´alayhis-Salaam) ujumbe wake haukuwa kwa watu wote. Ujumbe wake ulikuwa kwa wana wa israaiyl pekee na hakutumilizwa kwa kwa watu wote. Nyujumbe zao zilikuwa ni maalum kwa ajili ya watu wao. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mtume alikuwa akitumilizwa kwa watu wake maalum na nimetumilizwa kwa watu wote.”

Muusa (´alayhis-Salaam) alitumilizwa kwa wana wa israaiyl pekee na hakutumwa kwa watu wote. Kwa hivyo haitakiwi kusema kwamba Khidhr alitoka katika Shari´ah ya Muusa. Kwa sababu kimsingi ni kwamba hakuwa katika Ummah wa Muusa mpaka isemwe kwamba alitoka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 179-180
  • Imechapishwa: 07/03/2019