138. Kupeana mkono peke yake au kukumbatiana pia?

Swali 138: Tunaona wakati wa tanzia kwamba watu wengi wanapotaka kutoa pole basi wanambusu yule mfiwa au wanamkumbatia. Wengine wanakemea jambo hilo na kusema tanzia ni kupeana mkono peke yake. Unasemaje juu ya hilo[1]?

Jibu: Bora wakati wa tanzia au wakati wa kukutana ni kupeana mkono. Isipokuwa kama yule aliyekuja kutoa pole au aliyekuja kufanya makutano amefika kutoka safarini. Katika hali hiyo imesuniwa pamoja na kupeana mkono kukumbatiana. Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa wakikutana basi hupeana mikono na wakifika kutoka safarini basi hukumbatiana.”

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/374).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 100
  • Imechapishwa: 21/01/2022