138. Dalili kwamba Mtume amekufa


Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Baada ya watu kufa, watafufuliwa. Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):

إِنَّكَ مَيِّتٌ وَإِنَّهُم مَّيِّتُونَ ثُمَّ إِنَّكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عِندَ رَبِّكُمْ تَخْتَصِمُونَ

“Hakika wewe ni utakufa na wao pia ni watakufa. Kisha hakika nyinyi siku ya Qiyaamah mbele ya Mola wenumtagombana.”[1]

MAELEZO

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi Allaah alipokamilisha dini na neema kupitia yeye ndipo akamfisha, jambo ambalo ni mwenendo wa Allaah juu ya viumbe Wake:

كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ

“Kila nafsi itaonja mauti.”[2]

Manabii na Mitume wengine wanaingia ndani ya ueneaji huu:

كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ

“Kila nafsi itaonja mauti.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikufa na akatoka katika dunia hii na kwenda kwa Mola Wake (´Azza wa Jall). Haya yamethibiti kwa maandiko, maafikiano na kipimo. Kuhusu maandiko ni maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّكَ مَيِّتٌ وَإِنَّهُم مَّيِّتُونَ ثُمَّ إِنَّكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عِندَ رَبِّكُمْ تَخْتَصِمُونَ

“Hakika wewe ni utakufa na wao pia ni watakufa. Kisha hakika nyinyi siku ya Qiyaamah mbele ya Mola wenumtagombana.”

Hapa Allaah anamweleza Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba atakufa:

إِنَّكَ مَيِّتٌ

“Hakika wewe ni utakufa… ”

Bi maana utakufa. Mwenye kufa huambiwa kuwa amekufa. Kuhusu ambaye ameshakufa husemwa ميْت kwa kukhafifisha. Amesema (Ta´ala):

أَوَمَن كَانَ مَيْتًا فَأَحْيَيْنَاهُ

“Je, aliyekuwa maiti kisha Tukamhuisha.”[3]

ميْت ni yule ambaye roho yake imetengana na kiwiliwili chake. Maiti (الْمَيِّت) ni yule ambaye atakufa katika mustakabali.

[1] 39:30-31

[2] 03:185

[3] 06:122

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 276
  • Imechapishwa: 15/02/2021