138. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa pili wa al-A´raaf

al-´Ayyaashiy amesema:

“al-Husayn bin Mihraan amehadithia kutoka kwa Abu ´Abdillaah ambaye amesema kuhusiana na maneno Yake:

وَأَقِيمُوا وُجُوهَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ

“Muzielekeze nyuso zenu katika kila sehemu ya kusujudu.”[1]

“Bi maana maimamu.”

Muhammad bin al-Fudhwayl amehadithia kutoka kwa Abul-Hasan ar-Ridhwaa aliyesema kuhusiana na maneno Yake:

يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ

“Enyi wana wa Aadam! Chukueni mapambo yenu katika kila swalah.”[2]

“Bi maana nguo.”

al-Husayn bin Mihraan ameeleza kutoka kwa Abu ´Abdillaah aliyesema:

“Bi maana maimamu.”[3]

Huu ni upotoshaji wa kukusudia juu ya Kitabu cha Allaah.  ash-Shawkaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Elekeeni Kwake katika swalah zenu kukielekea Qiblah katika msikiti wowote mliopo au katika wakati wowote na sehemu yoyote mnaposujudu.

Makusudio ya mapambo ni yale mavazi wanayojipamba nayo watu. Amewaamrisha watu wavae vizuri wakati wanapoenda misikitini kwa ajili ya swalah. Aayah imetumiwa kama dalili vilevile juu ya uwajibu wa kusitiri viungo visivyotakiwa kuonekana katika swalah. Haya ndio maoni ya wanachuoni wengi.”[4]

 Makengeusho haya ya ki-Baatwiniy hayana malengo mengine isipokuwa ni njama ya kukipotosha Kitabu cha Allaah na kuwafanya wale wajinga wa Shiy´ah kuwa na msimamo wa kupindukia kwa maimamu wao, kuyaabudu makaburi yao na kuyatengua malengo na hukumu za Qur-aan.

Ni vipi zilikuwa hali za waislamu, katika Maswahabah na wengineo ambao wamezungumzishwa kwa Aayah hii, kabla ya kuzaliwa maimamu? Je, ni jambo linaloingia akilini kwamba Allaah amewaamrisha maimamu kuvaa mavazi mazuri wanapoenda katika kila swalah? Huu ni uzushi mkubwa unaokataliwa na akili na uhalisia wa mambo.

[1] 07:29

[2] 07:31

[3] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (2/12).

[4] Fath-ul-Qadiyr (2/244-246).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 197-198
  • Imechapishwa: 31/08/2018