137. Wafiwa kupanga safu wakati wa kuwapa mkono wa pole

Swali 137: Baadhi ya wale wenye kutoa pole wanawatoa nje wafiwa wa maiti mbali na makaburi na wanawapanga katika safu ili wawatambue na wawape pole kwa mpangilio na sababu nyingine ni ili makaburi yasitwezwe. Ni ipi hukumu ya hayo[1]?

Jibu: Sitambui ubaya wowote juu ya hayo. Kufanya hivo kunawasahilishia wale wahudhuriaji kuwapa pole.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/373-374).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 99-100
  • Imechapishwa: 19/01/2022