137. Vijitabu viwili vya Ibn Taymiyyah kuhusu Khidhr

Jambo la ajabu ni kwamba kuna kijitabu kinachonasibishwa kwa Shaykh-ul-Islaam bin Taymiyyah ndani yake kuna kwamba Khidhr yuko hai. Kmechapishwa ndani ya “Majmuu´-ar-Rasaa-il”[1] kwa kukosea. Sambamba na hilo ni kwamba ameandika kijitabu kingine kinachopinga kwamba Khidhr yuko hai ambacho nacho pia kimo ndani ya “Majmuu´-ul-Fataawa”[2]. Kijitabu hiki ambacho kimenasibishwa kwa Shaykh kuhusu kwamba Khidhr yuko hai si cha kweli. Hata kama kitakuwa ni cha kweli ni makosa. Kinachozingatiwa ni kile kijitabu chake cha pili ambacho kinaafikiana na dalili. Mtu akiwa na kauli mbili; moja wapo inaafikiana na dalili na nyingine inakwenda kinyume na dalili, basi itachukuliwa kauli ile inayoafikiana na dalili.

[1] Majmuu´ al-Fataawa (4/338)

[2] Majmuu´ al-Fataawa (4/337)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 179
  • Imechapishwa: 07/03/2019