137. Maafikiano juu ya kwamba Mtume amekufa


Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule atakayefanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu atarudishiwa mwenyewe.”[1]

Tahadharini na mambo yaliyozuliwa. Kwani hakika kila kilichozuliwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu.”[2]

Yule ambaye anazusha ´ibaadah mbalimbali zisizokuwa na dalili kutoka katika Qur-aan wala kutoka katika Sunnah za Mtume wa Allaah basi ameituhumu dini hii kwamba haikukamilika na yeye eti anataka kuikamilisha dini hii kutoka kichwani mwake na kwamab yeye hatambua Allaah kumkamishia yeye dini. Yale ambayo hayakuwa ni dini wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hayawezi hata siku moja baada yake kuwa ni dini. Hii ni Radd juu ya mapote haya. Pote la kwanza ni lile linalosema kuwa Uislamu hausilihi katika kila zama au wale wanaozua Bid´ah na mambo yaliyozuliwa ambayo hayana dalili kutoka katika Qur-aan na Sunnah na isitoshe wakazinasibisha katika dini. Basi katika Aayah hii kuna Radd juu yao. Kwani dini imeshakamilishwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Hivyo hakuna nafasi ya kuzidisha wala kupunguza kama ambavo hakuna nafasi ya kubabaisha na kutatiza kwamba haisilihi kwa watu waliokuja katika zama za mwisho:

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ

”Leo nimekukamilishieni dini yenu… ”[3]

Haya ni maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ambaye ndiye mkweli kabisa. Vilevile amesema:

وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا

“… na nimekutimizieni neema Yangu na nimekuridhieni kwenu Uislamu uwe ndio dini yenu.”[4]

Haya ni ya mwisho yaliyoteremka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni ushuhuda kutoka kwa Mola wa walimwengu kwa dini hii juu ya utimilifu, ueneaji wake  na kusilihi kwake katika kila zama na kila mahali. Maneno Yake (Ta´ala) ni utamkishaji juu ya Ummah huu kuanzia wa mwanzo wao mpaka wa mwisho wao. Sio utamkishaji wa kizazi cha kwanza peke yake. Ni utamkishaji juu ya kila Ummah hadi kisimame Qiyaamah.

Kuhusu maafikiano Ummah umeafikiana juu ya kufariki kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakuna waliokwenda kinyume na msimamo huo isipokuwa makhurafi wanaosema kuwa Mtume hakufa na wanapinga kifo juu ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haya ni maneno ya kipuuzi na yenye kurudishwa waziwazi. Ni maneno yanayorudishwa na hisia na uhalisia wa mambo. Hakika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikufa kati ya Maswahabah zake ambapo wakamuosha, wakamvika sanda, kumswalia na wakamzika (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Je, matendo haya hufanyiwa mtu amabye yuhai? Alifanyiwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama wanavofanyiwa waliokufa; alioshwa, akavikwa sanda na akazikwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndani ya kaburi lake. Huu ndio mwenendo wa Allaah juu ya viumbe Wake. Isitoshe wako wapi Mitume wengine waliokuwa kabla yake? Mwenendo juu yake ni uleule wa Mitume wengine kabla yake. Wamekufa na yeye ni mmoja katika wao. Hili ni kwa maafikano ya Ahl-us-Sunnan wal-Jamaa´ah. Hawakwenda kinyuume na haya isipokuwa tu makhurafi ambao wanamtegemea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wanamtaka msaada badala ya Allaah na wanasema kuwa yuko hai.

[1] al-Bukhaariy (7350) hali ya kuiwekea taaliki na Muslim (18) (1718).

[2] Abu Daawuud (4607), at-Tirmidhiy (2676), Ibn Maajah (42, 43), Ahmad (28/373) (17144).

[3] 05:03

[4] 05:03

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 274-276
  • Imechapishwa: 15/02/2021