136. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa kwanza wa al-A´raaf

al-´Ayyaashiy amesema:

“Abu Baswiyr amepokea kutoka kwa Abu ´Abdillaah ambaye amesema:

قَالَ فَبِمَا أَغْوَيْتَنِي لَأَقْعُدَنَّ لَهُمْ صِرَاطَكَ الْمُسْتَقِيمَ ثُمَّ لَآتِيَنَّهُم مِّن بَيْنِ أَيْدِيهِمْ وَمِنْ خَلْفِهِمْ وَعَنْ أَيْمَانِهِمْ وَعَن شَمَائِلِهِمْ ۖ وَلَا تَجِدُ أَكْثَرَهُمْ شَاكِرِينَ

“Akasema: “Basi kwa kuwa Umenihukumia kupotoka, nitawakalia katika njia Yako iliyonyooka, kisha nitawaendea mbele yao na nyuma na kuliani kwao na kushotoni kwao na wala hutopata wengi wao ni wenye kushukuru.”[1]

“Njia ambayo Ibliys anaizungumzia ni ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh).”[2]

Allaah amemtakasa Abu ´Abdillaah kutokamana na uongo na upumbavu huu. Njia iliyonyooka ni Uislamu ambao Allaah ameuweka tokea wakati wa Aadam mpaka wakati wa Mtume wa mwisho (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] 07:16-17

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (2/9).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 196
  • Imechapishwa: 31/08/2018