135. Ujumbe wa Muhammad ni kwa viumbe wote; watu na majini

Hakika ujumbe wake ni kwa watu wote na dini yake inafuta dini zengine zote. Hapakubali dini baada ya kutumwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) isipokuwa dini ya Kiislamu aliyokuja nayo. Kwa ajili hiyo ´Iysa (´alayhis-Salaam) atapoteremka atamfuata Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuhukumu kwa Shari´ah ya Uislamu na atakuwa ni mwenye kumfuata Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakuna katika watu na majini yeyote anaweza kutoka katika Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَإِذْ صَرَفْنَا إِلَيْكَ نَفَرًا مِّنَ الْجِنِّ يَسْتَمِعُونَ الْقُرْآنَ فَلَمَّا حَضَرُوهُ قَالُوا أَنصِتُوا ۖ فَلَمَّا قُضِيَ وَلَّوْا إِلَىٰ قَوْمِهِم مُّنذِرِينَ قَالُوا يَا قَوْمَنَا إِنَّا سَمِعْنَا كِتَابًا أُنزِلَ مِن بَعْدِ مُوسَىٰ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ وَإِلَىٰ طَرِيقٍ مُّسْتَقِيمٍ يَا قَوْمَنَا أَجِيبُوا دَاعِيَ اللَّـهِ وَآمِنُوا بِهِ يَغْفِرْ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُجِرْكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ  وَمَن لَّا يُجِبْ دَاعِيَ اللَّـهِ فَلَيْسَ بِمُعْجِزٍ فِي الْأَرْضِ وَلَيْسَ لَهُ مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءُ ۚ أُولَـٰئِكَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ

”Wakati Tulipowaelekeza kwako kundi miongoni mwa majini wakisikiliza Qur-aan, walipoihudhuria walisema: “Nyamazeni [msikilize]!” Ilipokwisha [kusomwa], waligeuka kurudi kwa watu wao wakiwaonya. Wakasema: “Enyi qaumu yetu! Hakika sisi tumesikia [kunasomwa] Kitabu kilichoteremsha baada ya Muusa hali ya kuwa kinayasadikisha yaliyo kabla yake, kinaongoza katika haki na katika njia iliyonyooka. Enyi watu wetu! Mwitikieni mlinganiaji wa Allaah na mwaminini hivyo Atakusameheni madhambi yenu na atakukingeni na adhabu iumizayo. Na yeyote yule asiyemuitikia mlinganiaji ya Allaah, basi hana uwezo wa kushinda katika ardhi na hatokuwa na walinzi badala ya Allaah – hao wamo katika upotofu wa wazi.” (al-Ahqaaf 72:29-32)

قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا

”Sema: “Nimeletewa Wahy kwamba kundi la majini lilisikiliza ambapo likasema: “Hakika sisi tumeisikia Qur-aan ya ajabu.” (al-Jinn 72:01)

Suurah “al-Jinn” yote ndani yake kuna yaliyosemwa na majini. Ujumbe wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kwa watu na majini wote. Yule asiyemuitikia na asimfuate, basi huyo ni katika watu wa Motoni kabisa, kwa sababu amemkufuru Allaah na Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wale wanaosema kuwa kuna yeyote anayeweza kutoka katika Shari´ah ya Mtume huyu ambapo wanatumia hoja juu ya hilo kwa kisa cha Khidhr na Muusa (´alayhis-Salaam). Kisa cha Khidhr kama alivyokitaja Allaah katika Qur-aan katika Suurah “al-Kahf” ya kwamba Muusa (´alayhis-Salaam) siku moja alikuwa anawakhutubia watu wake ambapo watu wake wakamuuliza:

“Hivi katika uso wa ardhi kuna ambaye ni mjuzi zaidi kuliko wewe?” Akajibu: “Hapana.” Ndipo Allaah (Ta´ala) akamwambia: “Mimi nina mja katika waja wangu katika ardhi fulani ambaye ana elimu usiyokuwa nayo.” Hivyo ndipo Muusa akaenda kwa mja huyo kutafuta elimu kwake. Amesema (Ta´ala):

وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِفَتَاهُ لَا أَبْرَحُ حَتَّىٰ أَبْلُغَ مَجْمَعَ الْبَحْرَيْنِ أَوْ أَمْضِيَ حُقُبً

”Pindi Muusa aliposema [kumwambia] kijana wake: “Sitaacha kuendelea mpaka nifikie zinapokutana bahari mbili au nitaendelee muda mrefu.”(al-Kahf 18:60)

Mpaka  alipofikia katika ardhi ambapo alikuwepo Khidhr. Akamwambia:

هَلْ أَتَّبِعُكَ عَلَىٰ أَن تُعَلِّمَنِ مِمَّا عُلِّمْتَ رُشْدًا

“Je, nikufuate ili unifunze katika yale uliyofunzwa ya busara?” (al-Kahf 18:66)

Anamuomba. Hakuja kwa ugumu na ukali. Bali mwanafunzi anatakiwa kufanya adabu na yule mwalimu wake:

هَلْ أَتَّبِعُكَ عَلَىٰ أَن تُعَلِّمَنِ مِمَّا عُلِّمْتَ رُشْدًا  قَالَ إِنَّكَ لَن تَسْتَطِيعَ مَعِيَ صَبْرًا

 “Je, nikufuate ili unifunze katika yale uliyofunzwa ya busara?” Akasema: “Hakika hutoweza kuvumilia pamoja nami.” (al-Kahf 18:66)

Mpaka mwisho wa kisa ndani yake kumetajwa kutobolewa safina, kumuua mtoto na kujengwa kwa ukuta. Akashangaa sana Muusa (´alayhis-Salaam) kwa kuwa haya ni mambo alikuwa hayajui. Alipombainishia Khidhr kwa nini alifanya mambo haya na kwamba haya ni kwa amri ya Allaah. Akasema:

وَمَا فَعَلْتُهُ عَنْ أَمْرِي

”Sikufanya hayo kwa amri yangu.” (al-Kahf 18:82)

Bali ni kwa amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Vilevile akamwambia Muusa:

“Mimi niko na elimu ambayo amenifunza Allaah ambayo wewe huna na wewe uko na elimu aliyokufunza Allaah ambayo mimi sina.”[1]

[1]Kisa hiki amekipokea al-Bukhaariy kwa namba. (74) na Muslim (2380).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 177-178
  • Imechapishwa: 07/03/2019