Shaykh Bakr amesema:

“Lakini kuna uwezekano ikawa ni kosa la mwanafunzi aliyekujia na taarifa hizi bila ya wewe kujua hilo.”

Sijui ni kipi anachokusudia kwa matusi haya. Ikiwa anakusudia kuwa mwanafunzi ndiye anayenisaidia katika kutunga, ni tuhuma za dhuluma ambazo Allaah atamfanyia hesabu kwazo. Huenda yeye na watu mfano wake ndio wanastahiki zaidi kutuhumiwa kwa kitu kama hicho. Mimi niko mbali kutokamana na hilo. Sintoridhia katu mtu anitungie neno hata moja. Njia yangu inajulikana vizuri sana na wenye busara na werevu.

Ikiwa anakusudia kuwa nasaidiwa kuandika vizuri baadhi ya maandiko, hiyo sio aibu. Kusaidiwa kuandika vizuri maandiko ni kama kusaidiwa na mashine ya kuchapisha. Anayejua anachokisema haonelei kuwa ni kasoro yoyote.

Nafikiria kuwa anachokusudia ni hizo tuhuma za kwanza na Allaah ni mwenye kumtosheleza. Mtu ambaye hamchi Allaah tu ndiye anayeweza kuja na tuhuma za kimakosa.