134. Ibn Baaz kuhusu kuhudhuria na kuketi katika vikao vya tanzia


Swali 134: Je, inafaa kuhudhuria vikao vya tanzia na kuketi pamoja nao[1]?

Jibu: Muislamu akihudhuria na akawapa pole wafiwa wa maiti ni jambo lililopendekezwa. Kufanya hivo kuna kuwaunga na kuwafariji. Hakuna neno akinywa hapo kwao kikombe cha kahawa au kitu kingine au manukato. Hivo ndivo zilivyo desturi za watu kwa wageni wanaokuja kuwatembelea.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/371).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 97
  • Imechapishwa: 18/01/2022