133. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa tano wa al-An´aam

al-´Ayyaashiy amesema:

“Yaziyd al-´Ijliy ameeleza kutoka kwa Abu Ja´far kwamba amesema:

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ

“Na kwamba hii ni njia Yangu iliyonyooka, hivyo basi ifuateni na wala msifuate njia za vichochoro zitakufarikisheni na njia Yake.”[1]

“Unajua:

صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا

“Njia Yangu iliyonyooka… “

nini maana yake?” Nikasema: “Hapana.” Akasema: “Ni uongozi wa ´Aliy na wasii. Unajua:

فَاتَّبِعُوهُ

“… hivyo basi ifuateni… “

nini maana yake?” Nikasema: “Hapana.” Akasema: “Maana yake ni kwamba mfuate ´Aliy bin Abiy Twaalib. Unajua:

وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ

“… na wala msifuate njia za vichochoro zitakufarikisheni na njia Yake.”

Nikasema: “Hapana.” Akasema: “Ninaapa kwa Allaah kwamba ni uongozi wa fulani na fulani. Unajua:

وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ

“… na wala msifuate njia za vichochoro zitakufarikisheni na njia Yake.”[2]

Nikasema: “Hapana.” Akasema: “Njia ya ´Aliy.”

Mhakiki amerejesha kwa “al-Bihaar”, “al-Burhaan”, “as-Swaafiy” na “Ithbaat-ul-Hudaat”.

Allaah amemtakasa Abu Ja´far al-Haashimiy kutokamana na uongo huu! Njia iliyonyooka ni Uislamu ambao amefikisha Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao ndani yake mna Qur-aan na Sunnah. Allaah amemwamrisha Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aweke wazi kwamba hafuati jengine isipokuwa Wahy ambao Allaah amemteremshia. Allaah (Ta´ala) amesema kumwambia Mtume huyu mkarimu:

قُلْ مَا كُنتُ بِدْعًا مِّنَ الرُّسُلِ وَمَا أَدْرِي مَا يُفْعَلُ بِي وَلَا بِكُمْ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ وَمَا أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ مُّبِينٌ

“Sema: “Mimi sikuwa jambo jipya lilozuka miongoni mwa Mitume na sijui nitakavyofanyiwa mimi wala nyinyi. Hakuna ninachofuata isipokuwa niliyoteremshiwa; nami si chochote isipokuwa ni mwonyaji wa wazi.”[3]

Allaah (Ta´ala) amemwamrisha kufuata Wahy anaoteremshiwa:

وَاتَّبِعْ مَا يُوحَىٰ إِلَيْكَ وَاصْبِرْ حَتَّىٰ يَحْكُمَ اللَّـهُ ۚ وَهُوَ خَيْرُ الْحَاكِمِينَ

“Fuata yale uliyoteremshiwa na subiri mpaka Allaah ahukumu. Naye ni mbora wa wanaohukumu.”[4]

Mtume mkarimu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Ummah wake vilevile waongozwa kwa mwongozo wa Wahy. Allaah (Ta´ala) amesema hali ya kumwamrisha:

قُلْ إِن ضَلَلْتُ فَإِنَّمَا أَضِلُّ عَلَىٰ نَفْسِي ۖ وَإِنِ اهْتَدَيْتُ فَبِمَا يُوحِي إِلَيَّ رَبِّي ۚ إِنَّهُ سَمِيعٌ قَرِيبٌ

“Sema: Ikiwa mimi nimepotea, basi nimepotea kwa kuidhuru nafsi yangu mwenyewe, na ikiwa nimeongoka, basi ni kwa sababu ya kunifunulia na Mola wangu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Aliye karibu.”[5]

Allaah (´Azza wa Jall) ameuamrisha Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuufuata Wahy huu na kusema:

اتَّبِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلَا تَتَّبِعُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ ۗ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ

“Fuateni yale mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wenu na wala msifuate badala Yake walinzi wengine – ni machache mnayoyakumbuka.”[6]

Ummah wote na ´Aliy ni mmoja katika wao wameamrishwa kukifuata Kitabu hiki na Mtume huyu mkarimu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kukitokea mzozo kati ya ´Aliy na mwengine, basi wote wameamrishwa kuhukumiana kwa Allaah na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amesema (Ta´ala):

وَهَـٰذَا كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ فَاتَّبِعُوهُ وَاتَّقُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ

“Na hiki Kitabu Tumekiteremsha hali ya kuwa ni chenye kubarikiwa, basi kifuateni na muogope ili mpate kurehemewa.”[7]

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا

“Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi; mkizozana juu ya jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamuamini Allaah na siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri kabisa.”[8]

Kukitokea mzozo kati ya ´Aliy na mwengine, basi wote wameamrishwa kuhukumiana kwa Allaah na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). ´Aliy hakukingwa na makosa. Ni vipi basi ataweza yeye ndiye njia ilinyooka, kama wasemavyo Baatwiniyyah? Ni vipi wale wanaodaiwa kuwa ni wasii watakuwa ndio njia iliyonyooka?

Tazama uzandiki huu pindi Raafidhwah wanamfanya ´Aliy na wale wanaodaiwa kuwa ndio wasii kwamba wao ndio njia iliyonyooka na wakati huohuo watu wabora zaidi baada ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wanawafanya wao ndio njia za vichochoro vinavyoelekeza katika upotevu na ukafiri unaofarikisha Ummah na kuzuia mbali na njia ya Allaah!

[1] 06:153

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/221).

[3] 46:09

[4] 10:109

[5] 34:50

[6] 07:03

[7] 06:155

[8] 04:59

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 190-191
  • Imechapishwa: 14/07/2018