132. al-Qummiy upotoshaji wake wa kumi na mbili wa al-An´aam

al-Qummiy amesema:

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ

“Na kwamba hii ni njia Yangu iliyonyooka, hivyo basi ifuateni… “

Njia ilinyooka ni imamu.

وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ

“… na wala msifuate njia za vichochoro… “

Bi maana, mwingine asiyekuwa imamu.

فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ

“… zitakufarikisheni na njia Yake.”[1]

Msitofautiana juu ya imamu. Mkitofautiana juu ya imamu basi mtapotea kutoka katika njia Yake. Hasan bin ´Aliy ametukhabarisha kutoka kwa baba yake, kutoka kwa al-Husayn bin Sa´iyd, kutoka kwa Muhammad bin Sinaan, kutoka kwa Abu Khaalid al-Qammaat, kutoka kwa Abu Baswiyr, kutoka kwa Abu Ja´far ambaye amesema:

“Sisi ndio njia. Yule mwenye kuikataa njia hii basi amekufuru.”[2]

Ajabu iliyoje ya upotevu huu, uongo na kujigonga! Allaah anakataza kufuata njia zengine na wao wanamnasibishia Abu Ja´far kwamba anasema kuwa wao ndio njia. Wapo ambao wamesema njia zengine ni Abu Bakr na ´Umar, jambo ambalo linakuja huko mbele.

[1] 06:153

[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/221).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 190
  • Imechapishwa: 03/07/2018