131. Je, ahukumiwe kifo ambaye ubongo wake umekufa?


Swali 131: Je, ahukumiwe kifo ambaye ubongo wake umekufa[1]?

Jibu: Asihukumiwe kufa na wala wasifanye haraka juu yake. Wasubiri mpaka pale atapokufa mauti yasiyokuwa na mashaka yoyote. Haraka hii wanakuwa nayo baadhi ya madaktari ili wapate kuchukua sehemu au viungo kutoka kwake. Wanacheza na kifo. Yote haya hayajuzu.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/366).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 95
  • Imechapishwa: 16/01/2022