131. al-Qummiy upotoshaji wake wa kumi na moja wa al-An´aam

al-Qummiy amesema:

“Kisha akamwambia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

قُلْ تَعَالَوْا أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ ۖ أَلَّا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا

“Sema: “Njooni nikusomeeni yale aliyoyaharamisha Mola wenu juu yenu; kwamba msimshirikishe na chochote na muwafanyie wema wazazi wawili.”[1]

Wazazi wawili ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kiongozi wa waumini.”

Tafsiri hii ni ya ajabu. Allaah kwenye Aayah nyingi za Qur-aan amekwishabainisha ni haki zipi alizonazo Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoamrisha atiiwe, akatahadharisha kutomkhalifu, akaamrisha kumsapoti na kumuheshimu na haki nyenginezo. Amebainisha vilevile haki za wazazi wawili, kukiwemo vilevile na Aayah hii. Hivi kweli Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ana haja Qur-aan ipotoshwe kwa ajili yake? Tazama namna ambavyo anamfanya ´Aliy kulingana na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)! Bali uhakika wa mambo ni kwamba hakukengeusha Aayah isipokuwa kwa ajili yake.

[1]  06:151

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 189
  • Imechapishwa: 03/07/2018