130. Fadhilah za Tasbiyh, Tahmiyd, Tahliyl na Takbiyr

  Download

254- Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule mwenye kusema:

سُبْحَانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ

“Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu na himdi zote njema ni Zake.”

kwa siku mara mia moja, basi hufutiwa makosa yake ijapo yatakuwa mfano wa povu la bahari.”[1]

255- Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule mwenye kusema:

لا إِلهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْد، وهُوَ عَلى كُلِّ شَيءٍ قَديرٌ

”Hapana mungu wa haki isipokuwa ni Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, ufalme na himdi zote njema ni Zake Naye juu ya kila jambo ni muweza.”

mara kumi, basi anakuwa kama ambaye ameacha nafsi nne katika wana wa Ismaa´iyl.”[2]

256- Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

 “Maneno mawili, mepesi kwenye ulimi, mazito kwenye mizani, yanayopendwa na Mwingi wa huruma:

سُبْحانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ سُبْحَانَ اللهِ العَظِيمِ

“Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu na himdi zote njema ni Zake na Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu Aliye mtukufu.”[3]

257- Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kusema:

سُبْحَانَ اللهِ، والحَمْدُ للهِ، وَ لاَ إِلَهَ إلاَّ اللهُ واللهُ أَكْبَرُ

“Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu na himdi zote njema ni Zake, hapana mungu wa kweli isipokuwa Allaah na Allaah ni mkubwa.”

kunapendeza zaidi kwangu kuliko kilichoangaziwa na jua.”[4]

258- Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hivi anashindwaje mmoja wenu kujichumia kila siku thawabu elfu moja?” Akamuuliza muulizaji katika wale waliokuwa wamekaa ni namna gani mtu anaweza kujichumia thawabu hizo elfu moja ambapo akajibu: “Aseme:

سُبْحَانَ اللهِ

“Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu.”

mara 100, ataandikiwa thawabu elfu moja au atafutiwa dhambi elfu moja.”[5]

259- Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

سُبْحَانَ اللهِ العَظِيمِ وبِحَمْدِهِ

”Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu, Aliye mtukufu, na himdi Zote njema ni Zake.”

 basi hupandiwa mti wa mtende Peponi.”[6]

260- Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ee ´Abdullaah bin Qays! Hivi nisikujulishe juu ya hazina miongoni mwa hazina za Peponi?” Nikaitikia: “Ndio, ee Mtume wa Allaah.” Akasema: “Sema:

لاَ حَوْلَ وَلا قُوَّةَ إِلاَّ باللهِ

“Hapana namna wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah.”[7]

261- Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Maneno yanayopendwa zaidi na Allaah ni manne:

سُبْحَانَ اللهِ، والْحَمْدُ للهِ، وَلاَ إِلَهَ إَلاَّ اللهُ واللهُ أَكْبَرُ

”Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu, himdi zote njema anastahiki Allaah, hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na Allaah ni mkubwa.”

Ni sawa kuanza na lolote lile katika hayo.”[8]

262- Kuna mbedui mmoja alikuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Nifundishe maneno nitakayoyasema ambapo akamjibu: “Sema:

لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ، اللَّهُ أَكْبَرُ كَبِيرًا، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ كَثِيرًا، وَسُبْحَانَ اللَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ، وَلا حَوْلَ وَلا قُوَّةَ إِلا بِاللَّهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ

“Hapana mungu mwengine wa haki isipokuwa ni Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika. Allaah ni mkubwa tena sana, himdi zote njema anastahiki Allaah tena nyingi  mno. Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu, Mola wa walimwengu. Hapana namna wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah, Mwenye nguvu zisizoshindika, Mwenye hekima.”

Mbedui yule akasema:

“Haya ni kwa ajili ya Mola wangu. Yako wapi yangu?” Akasema:

اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي، وارْحَمْنِي، واهْدِنِي، وارْزُقْنِي

“Ee Allaah! Nisamehe, nirehemu, niongoze na niruzuku.”[9]

263- Pindi mtu alipokuwa anaingia ndani ya Uislamu basi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) humfunza swalah kisha anamwamrisha aombe kwa maneno yafuatayo:

اللَّهُمَّ اغْفِرِ لِي، وارْحَمْنِي، واهْدِنِي، وعَافِنِي وارْزُقْنِي

“Ee Allaah! Nisamehe, nirehemu, niongoze, niafu na niruzuku.”[10]

 264- “Hakika du´aa bora ni:

الْحَمْدُ للهِ

“Himdi zote njema anastahiki ya Allaah.”

na Dhikr bora ni:

لاَ إِلَه إِلاَّ اللهُ

”Hapana mungu wa haki isipokuwa ni Allaah.”[11]

265- “Mema yanayobaki daima ni:

سُبْحَانَ اللهِ، والْحَمْدُ للهِ،لاَ إِلَهَ إَلاَّ اللهُ واللهُ أَكْبَرُ  وَلاَ حَوٍلَ وَلا قُوَّةَ إِلاَّ باللهِ

”Himdi zote njema anastahiki ya Allaah, himdi zote njema ni stahiki ya Allaah, hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, Allaah ni mkubwa, hapana namna wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah.”[12]

[1] al-Bukhaariy (07/168) na Muslim (04/2071). Tazama ”Fadhilah zake nyenginezo kwa yule atakayeyasema mara mia moja pale anapoamka asubuhi na anapoingiliwa na jioni”, uk. 65 katika kitabu hiki.

[2] al-Bukhaariy (07/67) na Muslim (04/2071) kwa tamko kama lake. Tazama ”Fadhilah zake nyenginezo kwa yule atakayeyasema mara mia moja pale anapoamka asubuhi na anapoingiliwa na jioni”, uk. 66 katika kitabu hiki.

[3] al-Bukhaariy (07/168) na Muslim (04/2072).

[4] Muslim (04/2072).

[5] Muslim (04/2072).

[6] at-Tirmidhiy (05/511) na al-Haakim (01/501) ambaye ameisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikiana naye. Tazama ”Swahiyh-ul-Jaami’” (05/531) na ”Swahiyh-ut-Tirmidhiy” (03/160).

[7] al-Bukhaariy pamoja na al-Fath (11/213) na Muslim (4/2076).

[8] Muslim (03/1685).

[9] Muslim (04/2072) na Abu Daawuud ambaye amezidisha: “Pindi mbedui yule alipogeuka na kuondoka zake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:

“Mikono yake imejaa kheri.” (01/220).

[10] Muslim (04/2073) na katika upokezi mwingine wa Muslim imekuja:

“Kwani hakika mambo haya yamekukusanyia dini na Aakhirah yako.”

[11] at-Tirmidhiy (05/462), Ibn Maajah (02/1249) na al-Haakim (01/503) ambaye ameisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikiana naye. Tazama “Swahiyh-ul-Jaami´” (01/362).

[12] Ahmad kwa nambari. (513) kwa mpangilio wa Ahmad Shaakir. Cheni ya wapokezi ni Swahiyh. Tazama “Majma’-uz-Zawaaid” (01/297). Ibn Hajar katika “Buluugh-ul-Maraam” ameiegemeza kutoka katika upokezi wa Abu Sa’iyd kwa an-Nasaa´iy na akasema:

“al-Haakim na Ibn Hibbaan wameisahihisha.”

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 09/05/2020