Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Atakayekuwa mgonjwa au safarini basi atimize idadi katika siku nyinginezo.”[1]

Ina maana kwamba ni wajibu kwake kulipa idadi ya zile siku alizokula pindi Ramadhaan inapoisha.

Ni wajibu ulipaji iwe kwa kufululiza au sio wajibu iwe hivyo? Kuna wanachuoni wachache waliosema kuwa ni wajibu kulipa kwa kufululiza. Wanachuoni wengi wamesema kuwa sio wajibu kulipa kwa kufululiza. Wanachuoni wengi katika Maswahabah na wengineo wanaonelea kuwa sio wajibu kulipa kwa kufululiza. Dalili ya hilo ni kwamba ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Nilikuwa na madeni ya siku za Ramadhaan. Sikuwa naweza kuyalipa isipokuwa katika Sha´baan kwa sababu nilikuwa nikishughulishwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[2]

[1] 02:185

[2] al-Bukhaariy (1950) na Muslim (1146).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tafsiyr Aayaat-is-Swiyaam, uk. 24-25
  • Imechapishwa: 02/06/2017