13. Vipi inatakiwa kuwaamini Mitume kwa njia ya upambanuzi?

Swali 13: Vipi mtu anatakiwa kuwaamini Mitume kwa njia ya upambanuzi?

Jibu: Ni juu yetu kuwaamini Manabii na Mitume wote ambao unabii na ujumbe wao umethibiti. Imani hii inatakiwa iwe kwa njia ya ujumla na upambanuzi.

Tunaamini kuwa Allaah amewateua kwa Wahy na kuwatumwa Kwake.

Amewafanya kuwa ni wakati kati baina Yake na viumbe Wake katika kufikisha dini na Shari´ah Yake.

Amewapa nguvu kwa alama zenye kuthibitisha kuwa ni wakweli na usahihi wa yale waliyokuja nayo.

Wao ndio viumbe wakamilifu kabisa inapokuja katika elimu, matendo, ukweli, wema na tabia.

Allaah amewakhusisha kwa fadhila walizopwekeka nazo na amewatakasa na kila sifa mbaya.

Wamekingwa na kukosea katika yale yote wanayofikisha kutoka kwa Allaah.

Hakuna kinachochukua nafasi katika maelezo na ufikishaji wao isipokuwa haki na ya usawa.

Ni wajibu kuwaamini wote na yale yote waliyopewa kutoka kwa Allaah. Vilevile ni wajibu kuwapenda, kuwaheshimu na kuwaadhimisha.

Tunaamini kuwa mambo yote haya ni wajibu kumtekelezea nayo Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa njia kamilifu zaidi.

Ni wajibu kumjua na kujua yale aliyokuja nayo katika Shari´ah kwa njia ya jumla na ya upambanuzi, kadri vile mtu atakavyoweza. Vilevile ni wajibu kuamini hilo, kushikamana nalo na kumtii katika kila kitu alichokielezea, kukiamrisha na kukikataza.

Yeye ndiye Nabii wa mwisho. Hakuna Nabii mwengine baada yake. Shari´ah yake imezifuta Shari´ah zingine zote na itaendelea kufanya kazi mpaka siku ya Qiyaamah.

Imani ya kumuamini haitimii mpaka mja atambue kuwa yote aliyokuja nayo ni haki.

Haiwezekani dalili ya kiakili, kihisia au nyengine ikapingana na yale aliyokuja nayo. Uhakika wa mambo ni kuwa akili timamu na mambo ya kihisia ya kihakika vyote viwili vinathibitisha kuwa Mtume ni mkweli na anazungumza haki.

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahamm-ul-Muhimmaat, uk. 73
  • Imechapishwa: 25/03/2017