Miongoni mwa elimu zilizozuliwa ni yale yaliyozuliwa na watu wa maoni (أهل الرأي) katika vidhibiti na kanuni za kutumia akili na kurudisha mambo ya mataga juu yake. Ni mamoja vigezo vyao vimeafikiana au vimekwenda kinyume na Sunnah, na hata kama watafasiri Qur-aan na Sunnah kujengea kanuni zao, lakini wametumia tafsiri ambayo wengine wanatofautiana nao. Haya ndio ambayo maimamu huko Hijaaz na ´Iraaq wamewakaripia watu wa maoni. Maimamu na wanachuoni wa Ahl-ul-Hadiyth ni wenye kufuata Hadiyth Swahiyh popote iwapo muda wa kuwa ilikuwa yenye kufanyiwa kazi na Maswahabah na waliokuja baada yao, au angalau kwa uchache kundi katika wao. Lakini haijuzu kufanyia kazi kile ambacho kuna maafikiano juu ya kukiacha, kwani hawakukiacha isipokuwa ni kwa sababu walitambua kuwa hakitakiwi kufanyiwa kazi. ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz amesema:

“Chukueni katika maoni yale yanayoafikiana na wale waliokuwa kabla yenu. Kwani wao walikuwa ni watambuzi zaidi kuliko nyinyi. Kuhusu zile Hadiyth zinazokwenda kinyume na matendo ya watu wa Madiynah, Maalik alikuwa akiona kuwa matendo ya watu wa Madiynah ni yenye kupewa kipaumbele.”

Ijapo jopo la waliokuwa wengi wameonelea Hadiyth ndizo zinazotakiwa kupewa kipaumbele.

  • Mhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Fadhwl ´Ilm-is-Salaf ´alaa ´Ilm-il-Khalaf, uk. 57
  • Imechapishwa: 20/09/2021