13. Hoja yaya ya waliokuja nyuma ndio ule ule wa washirikina wa kale

Hoja tata ya watu hawa waliokuja nyuma ndio hoja tata ileile ya wale wa kale. Utata wenyewe wanasema kuwa wawaombao ni waombezi wao mbele ya Allaah na kwamba hawawaombi isipokuwa ili wawakurubishe kwa Allaah. Allaah amebatilisha hoja tata hii na kubainisha kuwa atayemwabudu asiyekuwa Yeye – yeyote awaye – amemshirikisha na amekufuru. Hivyo ndivyo alivyosema (Ta´ala). Allaah (Subhaanah) amewaraddi kwa kusema:

وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَـٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللَّـهِ

“Wanaabudu asiyekuwa Allaah ambao hawawezi kuwadhuru na wala hawawezi kuwanufaisha na wanasema: “Hawa ni waombezi wetu mbele ya Allaah.”” (39:03)

Allaah (Subhaanah) akawaraddi kwa kusema:

إِنَّ اللَّـهَ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ فِي مَا هُمْ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي مَنْ هُوَ كَاذِبٌ كَفَّارٌ

“Hakika Allaah atahukumu baina yao katika yale waliyokhitilafiana nayo. Hakika Allaah hamwongoi aliye muongo, kafiri.” (39:03)

Katika Aayah hii amebainisha (Subhaanah) kuwa kumuabudu asiyekuwa Yeye katika Mitume, mawalii na wengineo, ya kwamba ni shirki kubwa. Haijalishi kitu hata kama mwenye kufanya hivo atayaita kwa majina mengine. Amesema (Ta´ala):

وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ

“Wale waliojichukulia badala Yake walinzi [wakisema]: “Hatuwaabudu isipokuwa ili watukurubishe kwa Allaah ukaribio.”” (39:03)

Allaah akawaraddi kwa kusema (Subhaanah):

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي مَنْ هُوَ كَاذِبٌ كَفَّارٌ

“Hakika Allaah hamwongoi aliye muongo, kafiri.” (39:03)

Amebainisha (Subhaanah) ya kwamba kule kuwaabudia kwao wengine kwa kuwaomba, kuwa na khofu kwao, kuwatarajia na mengineyo ni kumkufuru (Subhaanah) na akawakadhibisha vilevile ya kwamba waungu wao wanawakurubisha Kwake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Marejeo: al-´Aqiydah as-Swahiyhah wa maa yudhwaadduhaa, uk. 12
  • Imechapishwa: 31/05/2023