Swali 13:  Baadhi ya wanawake ambao wanaavya mimba hawatoki nje ya hali mbili:

1- Mwanamke aporomoshe mimba kabla ya kuumbwa kipomoko.

2- Mwanamke aporomoshe mimba baada ya kuumbwa kipomo na kuonekana mikakati yake.

Ni ipi hukumu ya kufunga katika kipindi kile ambacho ameavya mimba na kufunga masiku ambayo anaona damu inatoka?

Jibu: Ikiwa kipomoko hakijaumbwa basi damu hiyo sio damu ya uzazi. Kutokana na hilo atatakiwa kufunga na kuswali na funga yake ni sahihi. Ikiwa kipomoko kimeshaumbwa basi damu yake inahesabika ni ya damu ya uzazi. Haifai kwake kuswali wala kufunga katika kipindi hicho.

Kanuni au kigezo katika masuala haya ni kwamba ikiwa kipomoko kimeshaumbwa basi damu hiyo inahesabiwa ni damu ya uzazi. Na kipomoko ikiwa hakijaumbwa basi damu hiyo haizingatiwi ni ya nifasi. Damu ikiwa ni ya nifasi basi ni haramu kwake yale ambayo ni haramu kwa wanawake wengine ambao wana damu ya uzazi. Ikiwa sio damu ya uzazi basi mambo hayo si haramu kwake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 14-15
  • Imechapishwa: 20/06/2021